Mashada - African Chat, Discussions, Blogs, Photos, Classifieds & More!
 
HOME Forums Chat Photos Blog Events Calendar Directory

Go Back   Mashada Forums > Music & Entertainment > Music > muziki na biso...our music
Reply
 
LinkBack Thread Tools Display Modes
(#1 (permalink))
Old
Junior Member
chibole is on a distinguished road
 
Posts: 16
Join Date: Jun 2007
Report Post
Default muziki na biso...our music - 06-30-2007, 10:12 AM

MUZIKI NA BURUDANI


Papa Wemba
Papa Wemba ni mzaliwa Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba munamo mwaka wa 1949 huko Lubefu (Kasai - DR Congo). Yeye ni wakabila la kikongo, na mcheza ngoma maluumu ya Soukous na mwanamziki hodari anaye sifika kwote Africa na hata kule ulaya.
Papa Wemba ni mmoja wapo wa wanamziki, wanjilishi wa kikundi cha Soukous band, Zaiko Langa Langa kilicho anjiliswa December 24, 1969 huko Kinshasa (mji-mkuu wa Democrasia ya kongo) pamoja na wanamziki wa Kongo kama, Nyoka Longo Jossart, Manuaku Pepe Felly, Evoloko Lay Lay, Teddy Sukamu, Zamuangana Enock, Mavuela Simeon, na wengine.
Huko Kongo mziki ulidhumuika nyakati za mwanamziki Franco Luambo na kundi lake maluumu la TPOK Jazz, Tabu Ley Rochereau's Afrisa, makundi mageni kama Les Grands Maquisards, Le Trio Madjesi, na mengine mageni kama Bella-Bella, Thu Zaina na Empire Bakuba, mdogo lakini akiimarika, Papa Wemba (akijulikana hizo enzi kama Jules Presley Shungu Wembadio), alichangiya sana mwaka wa 1973 kuundwa kwa kikundi cha Zaiko Langa Langa kikundi changamfu na hodari, likiporomosha miziki kama "Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na " Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge Gina) na "Zania" (Mavuela Somo).
Munamo mwaka wa 1974, katika mchezo uliyoitwa “pinnacle of the fame (mwezi mmoja kabula ya mchezo mwingine wa Rumble in the Jungle kati ya mupiganji ndondi Muhammad Ali na mpinzani wake George Foreman kule Kinshasa), Shungu Wembadio (Papa Wemba), na Evoloko Lay Lay, Mavuela Somo na Bozi Boziana (waliohamiya Zaiko Langa Langa hapo mwanzoni), waliliwacha kundi laZaiko Langa Langa na kulianjilisha kundi lingine la Isifi Lokole, ISIFI ikiwa kikundi cha "Institut de Savoir Ideologique pour la Formation des Idoles."
Mwaka wa July 1975, Shungu Wembadio alijikakamua akilitumia jina lake la Papa Wemba, nyongesa ya "Papa" (baba) jukumu alilolichukua baada ya wazazi wake kuaga mwaka wa 1960s.
Muziki wa "feux d'artifice" (fireworks) ukiwa wa Isifi Lokole ulisifika kwa mwaka mmoja tu. Na mziki moja wa "Amazone" (Papa Wemba) ukieneya. Novemba 1975, Papa Wemba, Mavuela Somo na Bozi Boziana waliacha Evoloko Lay Lay na Isifi Lokole kuanza kikundi cha Yoka Lokole (pia likijulikana kama Kinshasha All-Stars, au Lokole Isifi, au Isifi), pamoja na mwanamziki Mbuta Mashakado, mmoja wapo wa mwanamziki wa kikundi cha Zaiko Langa Langa 'transfusion.' Yoka Lokole walinawiri kimuziki kuliko hata walivyo kua na kundi lakwanza la Isifi Lokole, lakini waliweza kubaki juu kwenye nyota ya mziki na nyimbo kama "Matembele Bangui", "Lisuma ya Zazu" (Papa Wemba), "Mavuela Sala Keba", na "Bana Kin" (Mavuela Somo).
Baada ya mwaka mmoja wakiimarika na ****nufaika, matatizo yalianza katika kundi la Yoka Lokole kuhusu fedha na maisha ya kifahali. (pamoja na kukamatwa kwa Wemba's na kufungu huko kinshasha Central prison munamo December 1976 kwa 'uhalifu' kujihuzisha kimwili na bintiye mwanajeshi mkuu, Papa Wemba, alidhulumiwa na mashabiki na baadaye akalianza kundi lingine la his Viva la Musica munamu Februari 1977.
Akiwa nyumbani kwake huko Matonge maeneo jirani ya Kinshasa, Papa Wemba aliliunda kundi la Viva la Musica akisaidiwa na wanamziki wengine kama Kisangani Esperant, Jadot le Cambodgien, Pepe Bipoli naPetit Aziza, mupiga gita wa Rigo Star, Syriana, na Bongo Wende. Kundi hili lilikua likianza kuimarika kimuziki, na nyimbo kama "Mere Superieure," "Mabele Mokonzi," "Bokulaka," "Princesse ya Sinza," na nyingine.
Akianza kuonyesha ushuja wake kati ya mwaka wa 1977, Papa Wemba'na familia yake walianza kusifika huku sifa zikieneya kumhuzu. Kutoka mwaka wa 1977,kikundi cha Viva la Musica lilikuwa limezidiwa na uhamaji wa wanamziki kila baada ya mia miwili au tatu kwa sababu ya makundi mengi madogo yaliyo kuja na ushanii na ushuja mbalimbali wa kimuziki. talents. King Kester Emeneya munamo miaka za (1977-1982), Koffi Olomide (1978-1979), Djuna Djanana (1978-1981), Dindo Yogo (1979-1981), Maray-Maray (1980-1984), Lidjo Kwempa (1982-2001), Reddy Amissi (1982-2001), Stino Mubi (1983-2001) kati ya wengi wanaojulikana,wote walipitia katika kundi la Viva la Musica. Katika hitoria hii, mwanafunzi mmoja wa shule ya utaluma aitwaye Antoine Agbepa Koffi alikuwa na ushupavu mwingi wa kuziandika miziki zilizowafurahisha wengi na munamo mwaka wa 1977 Papa Wemba akasika akizisifu na kusema, "Ooh! l'homme idee" (Oh! the idea-man!) papo hapo jina la mwanafunzi huyu likabadilika na akaanza kuitwa Koffi 'Olomide'--!
Baada ya mabadilko makuu ya usafiri katika inchi za uropa yaliyofanywa mwaka wa 1990s, Wemba alibaki na kundi moja (liitwalo wakati mwingine kama "Nouvelle Ecriture," "Nouvel Ecrita," na sasa tena "Viva la Musica") na lingine huko paris ("Nouvelle Generation," "La Cour des Grands," sasa linaloitwa "Viva Tendance").
Amebaki shuja na mwanamziki mwenye ujuzi wa hali ya juu na nyimbo kama "L'Esclave" (1986), "Le Voyageur, Maria Valencia" (1992), "Foridoles, Dixieme Commandement" (1994), "Emotion" (1995), "Pole Position" (1996), "Fula Ngenge" (1999), "Bakala dia Kuba" (2001),na "Somo Trop" (2003). Ni wengi muno katika bara la africa na hata kwingineko,ambao watazidi kumhesimu mziki wa Wemba "shuja," kama wengi wanao zidi kumpa sifa mwanamziki(Franco Luambo, Tabu Ley Rochereau, na Miriam Makeba kati ya wengi.
Papa Wemba pia anajulikana kama msani.munamo mwaka wa 1987, alicheza katika filama moja ya kunawiri kwa Zaire (Kongo) film La Vie est. na muzungu mmoja wa Kibelgiam mkurugensi Benoit Lami na Ngangura Mweze.


Utafiti umefanywa na Simon Chibole, sanduku la posta: 7577 Eldoret. Rununu:0720220987 au barua pepe kwa: tsammie76@yahoo.com
 
Reply With Quote
Reply


Thread Tools
Display Modes

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

vB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are On
Pingbacks are On
Refbacks are On






SEO by vBSEO 3.1.0