RE: # 9 AREA CODE EASTLEIGH MASSIVE -
05-14-2005, 02:41 AM
Maze mabeste nimesoma hizi risto za easich mpaka nikaskia nostalgia ingine hapo......Mi, wasee ni mmoja wao. Easich foreee. First Tulikua tunapoa hapo hivyo stage inaitwa "Blueband" right by Muyuyu alafu unapanda ka two blocks mpaka ploti fulani ilikua na migomba za ndizi. Kuna msee ali-mention akina mureithi, akina Isa...hao wote walikua ma-neighbor. Niliendanga primo Racecourse time za akina Githesh, Mule, Wambua(shrubbist) proper,Gachie, Rono,Alumasa(alikua na mkidi dosho supu mbaya alikua anaitwa Gail),Kioko(R.I.P- best headmaster i have ever had), Mr. Mbihane(alikua na kiboko ya pipe, akikuchapa nayo inalia oboboo!)Kibuchi etc.
Jamaa mnakumbuka piko iki-come mlikua mna-shine mngaro ile uko nayo best.Wale walikua wameosa walikua wana buy sambusa, mabuyu, maembe ama ice cream mob, alafu ka wewe umecharara ulikua unastay mbali na canteen(kuna msee alikua kwa hiyo canteen alikua anaitwa ndyson,shrub for tyson). ama ukiget report card unaishia home speedi wasee wasimesee ati hauna any. Alafu unakumbuka maodijo walikua wanabuy kuku mob siku ya piko(picnic)alafu ma-fovorite "pupils" ndio wanabakia wakisaidia kuzichinja.
Nani anakumbuka tulikuanga na "team". I guess ivo ndio walikua wakiita ka mnaenda kucheza na team ya chuo ingine. sisi Racecourse tulikua tumechukia pango mbele walikua maoboho alafu walikua wanatushinda all the time. Juja primo was our favorite mbele tuilkua tunawafanya 24/7.Nani anakumbuka debate? "NAOMBA WAPINZANI WAVUKE SAKAFU MWENDO WA KIASTE ASTE, MWENDO WA KINYONGA, WATUUNGE KATIKA HUU MJADALA USEMAO WHISKI NI BORA KULIKO BIA"
Nanianakumbuka yusuf madogi? kuna msee ali-mention makudinyo.mpaka saa hii vile naandika bado nacheka vile wasee bado wankumbuka msee ka huyo.
Nani ankumbuka hizi mathree......Ladies edition(kuna makanga wa hii mathree beste ya mine sana nimemsahau jina, alkua mfupi alikua mkatiaji noma. Alikua Senti seco alafu aka-drop out) Kappa, Blackstreet,Lost Boyz?? nakumbuka tulihama alafu stage yangu ya kushuka ilikua Marie stopes. Kulikua na place ya video kurentisha inaitwa Boomerang apo ivyo. Maze ma-memoriez ni mob siskii kuacha kuandika.
|