just a shairi -
08-04-2005, 07:06 PM
Kaniaga Kwaheri:
Namkumbuka, namwona mawazoni,
kasimama imara hapo barabarani,
na machozi tele,
kamtoka machoni,
sijui kama nitawahi tena,
kupenda, nilivyompenda,
kwani kila nilipomtazama,
moyo ulibubujika waama,
na sasa...,
moyo ushakufa ganzi,
sina hisia wala kumbukumbu,
kaufunga moyo na kuutupa ufunguo mbali,
mapenzi yakawa kizungumkuti kwangu,
jina baridi tu, mithili ya barafu,
jina ambalo linachoma roho,
na kuuwacha ukiteketea,
mapenzi huja na mapenzi hufutuka,
mapenzi ni kufa na kupona,
na uponapo, ufe tena mara ya pili.
Written by caroline ndambuki
©.all rights reserved ® creativewriteworks
|